Sukari (Diabetic)
Nilianza kuwa na dalili za kudhoofika afya. Nilipopima nikagundulika nina Kisukari.
Changia leo, okoa maisha yangu.
Wimbo hapo juu nimaalum aliouimba Gadi Sedekia
Mimi ni Gadi Sedekia. Hali yangu ya afya siyo nzuri, kwa sababu sipati haja ndogo. Figo zangu zote hazifanyi kazi. Kwa msaada wa mashine maalum za kuondoa sumu mwilini ninaishi, ila kwa maumivu makali sana.
Sadaka yako nitumie moja kwa moja kwenye akaunti zangu(Gadi Sedekia) kama ifuatavyo:
Mahojiano kati ya Gadi Sedekia na Sales Silayo wa Simulizi na Sauti, Arusha Tanzania.
Sukari ilianza kunisumbua nikiwa na miaka 19. Kisha likafuata shikizo la damu, na sasa imepelekea figo kushindwa kufanya kazi. Nilipambana na kumudu kuishi kwa uzoefu na kuwasaidia wengine waliokata tamaa hasa waliosumbuliwa na ugonjwa wa Sukari.
Nilianza kuwa na dalili za kudhoofika afya. Nilipopima nikagundulika nina Kisukari.
Baada ya changamoto nyingi, nilihisi kuchoka zaidi ya vile nilivyozoea. Nilipima Hospitalini nikagundulika nina shinikizo la Damu, yaani Presha
Daktari alipoona hali yangu inazidi kuwa mbaya alinianzishia dawa na kupewa ushauri wa kitabibu ili kupambana na magonjwa mawili, Sukari na Presha.
Hali ilizidi kuwa mbaya, miguu ikavimba sana, kumbe figo zinaleta shida. Nikaanza kufanyiwa Dialysis. Mount Meru Hospital, Arusha.
Nikafanyiwa upasuaji mdogo wa kupandikiza king’amuzi cha kusaidia kufanya Dialysis.
Maendeleo yangu yakazidi kuwa mabaya hadi kufanya Dialysis Mara TATU kwa wiki
Niliwasiliana na Familia na kuamua kutafuta msamalia wa kunisaidia Figo, wakapatikana, na sasa nahitaji Mchango ili nifanikishe matibabu
Ugonjwa ulianza nikiwa kidato Cha Sita nikikaribia kumaliza. Niliendelea na maisha ya shule nikiwa na Sukari. Na sasa napambana na Dialysis. Naomba mchango wako ili kupandikiza Figo.
Kupandikizwa figo ni tiba bora kuliko dialysis ya muda mrefu, lakini inahitaji ufuatiliaji wa karibu na matumizi ya dawa za kudhibiti kinga maisha yote.
Mtu hupandikizwa figo pale figo zake zimeharibika kabisa na haziwezi tena kufanya kazi ya kuchuja damu, kutoa sumu mwilini, na kudhibiti maji na chumvi. Hii mara nyingi hutokana na ugonjwa sugu wa figo (chronic kidney disease) au figo kushindwa kabisa kufanya kazi (end-stage renal disease).



Gadi ni kijana mdogo, ana umri mdogo na bado ana ndoto nyingi sana. Kwa sasa ana matumaini makubwa ya kutimiza ndoto zake hasa zinazohusiana na kusaidia jamii. Anahisi kuwa bado kuna mambo makubwa au ndoto kubwa ya mambo ya kutimiza katika jamii na dunia kwa ujumla. Hebu tuangalie kidogo kazi zake za mziki wa injili na huduma za jamii ambazo ni sehemu ya ndoto zake;
Kupandikiza figo hutoa faida kubwa kiafya kwa wagonjwa wenye kushindwa kwa figo, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa muda wa kuishi, ubora wa maisha, na uhuru kutoka kwa mashine za dialysis. Ni tiba bora zaidi kuliko dialysis kwa wagonjwa wengi wa ugonjwa wa figo wa hatua ya mwisho.
Faida za Kupandikizwa Figo ni hizi hapa;



Mchango wako wa matibabu ni muhimu kwa sababu gharama za matibabu ni kubwa na siwezi kuzifikia kwa urahisi peke yangu.
Hapa kuna sababu kuu kwa nini mchango wako wa matibabu ni wa maana sana kwangu:
Upandikizaji wa figo mara nyingi ni suluhisho pekee kwa wagonjwa wenye figo kushindwa kufanya kazi. Bila msaada huu, wagonjwa wengi hutegemea dialysis maisha yote, ambayo ni ngumu na yenye gharama kubwa.
Dialysis inachosha mwili na akili. Figo jipya linaweza kumruhusu mgonjwa kuishi maisha yenye afya na uhuru zaidi.
Upandikizaji wa figo ni mchakato wa kitabibu unaohitaji vifaa, madaktari bingwa, dawa za kupunguza kinga, na ufuatiliaji wa muda mrefu. Michango husaidia kufidia gharama hizi ambazo mara nyingi mgonjwa peke yake hawezi kumudu.
Ni Mtu akipata figo jipya na kupona, anaweza kurudi kazini, kusaidia familia yake, na kuchangia maendeleo ya jamii.
Kuchangia ni tendo la huruma na mshikamano wa kijamii. Ni njia ya kuonyesha upendo na mshikamanio kwa wale wanaopitia changamoto kubwa kiafya. s
Kwa kifupi, kuchangia fedha ya kupandikiza figo ni kuchangia maisha mapya na matumaini mapya.
Familia hupata nafuu kwa sababu mgonjwa anakuwa na afya bora na si tegemezi sana.
Pia atapona, na kurudi kazini, kusaidia familia yake, na kuchangia maendeleo ya jamii.

Kanuni za Utoaji wa Kibiblia zinatutaka tutoe namna hii;